Monday 5 December 2016

YARA MILA COMPLEX
Mkulima mzuri ni yule annayekubali ushauri..
YARA TANZANIA LTD ni chachu ya maendeleo ya mkulima
katika msimu huu wa kilimo, mkulima wa kitanzania chaguo lako sahihi ni Mbolea bora kutoka YARA (T) LTD
Mifuko 3 ya YARA MILA CIRIO kwa ekari moja unapata mavuno ya kutosha.
Lima kilimo cha kisasa cha kibiashara kwa kutumia mbolea kutoka kampuni ya yara.

Saturday 5 March 2016

KILIMO BORA CHA NYANYA



Info Post
6/26/2015 09:25:00 AM

Utangulizi:


Kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na pia kama zao la biashara nyanya hulimwa sehemu nyingi duniani . Asili yake ni nchi ya Peru/Equador huko Amerika ya Kusini. Mmea huu ulianza kuzalishwa kama zao katika nchi ya Mexico na baadaye kusambaa katika nchi nyingine za ulimwengu.
  1. Aina ndefu ( intermediate) kwa mfano ANNA F1, Tebgeru 97. Aina hizi hufanya vizuri zaidi zinapopandwa ndani ya greenhouse. Aina hii Uvunaji wake ni wa muda mrefu, zipo ambazo zinavunwa hata zaidi ya miezi 6, yaani hiyo miezi 6 ni ya uvunaji.
  1. Aina fupi (determinate) kwa mfano Tanya, Cal J, Mwanga, Onyx, Roma VF (nyanya mshumaa)
  1. 1. OPV (Open Pollinated Variety) - Aina za kawaida
  1. 2. Hybrid – Chotara: Hizi ni aina zenye mavuno mengi, kati ya hizo zipo aina fupi na ndefu.Nyanya zinazopendelewa kulimwa zaidi na wakulima, ni zile zinazoweza kuvumilia magonjwa na kuzaa sana, na zenye ganda gumu ili kufanikisha usafirishaji, na kuhifadhika kwa siku nyingi bila kuharibika mapema.

  • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu
  • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha
  • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo.
  • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.)
  • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine.
  • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche].
  • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini.
  • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma 4-8 ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu.
  • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo.
  • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba.
  • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota.

  • matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi.
  • mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi
  • matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara.
  • Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri.
  • matuta haya ni rahisi kutengeneza
  • hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu
  • nyevu mdogo unaopatikana ardhini
  • ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba
  • huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu
  • huzuia mmomonyoka wa ardhi
  • Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye
  • mvua nyingi.
  • ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa
  • na kusambazwa mbegu huoteshwa
  • ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu
  • Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi.
  • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
  • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
  • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
  • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
  • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
  • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
  • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
  • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
  • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
  • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
  • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
  • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.
  • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
  • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
  • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
  • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
  • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
  • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
  • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
  • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.
Maandalizi ya Shamba la Nyanya
  • Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
  • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
  • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
  • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.
  • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
  • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
  • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
  • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.
  • Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
  • Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
  • Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
  • Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.


Uzalishaji wa nyanya hapa Tanzania na kwingine


Nchi zinazolima nyanya kwa wingi duniani ni pamoja na Marekani, Italia na Mexico. Kwa upande wa Afrika nchi zinazo lima ni kama; Malawi, Zambia na Botswana. Zao hili hulimwa pia katika nchi za Afrika Mashariki, ikiwemo Kenya, uganda na Tanzania.


Tanzania hulimwa maeneo mengi kwa nia kukidhi mahitaji ya kaya na biashara pia. Uzalishaji wa nyanya ni mkubwa kuliko mazao mengine ya mbogamboga yanayolimwa hapa Tanzania, uzalishaji wa nyanya kwa mwaka ni zaidi ya tani 129,578 ikiwakilisha asalimia 51 ya mazao yote ya mboga. Kwa mujibu wa Wizara ya kilimo, chakula na ushirika Tanzania maeneo yanayolima sana nyanya ni pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro (Hai, Moshi na Rombo), Arusha (Arumeru), Morogoro (Mgeta), Tanga (Lushoto), Mbeya (Mbeya vijijini), Njombe, Iringa na Singida. Morogoro ndiyo inayoongoza kwa kilimo hichi ikiwa na wazalishaji wenye zaidi ya hekta 6,159 ambazo ni sawa na zaidi ya ekari 15,398. Pamoja na kwamba eneo la uzalishaji linaongezeka kwenye maeneo mengi lakini uzalishaji wa nyanya bado ni mdogo sana kutokana na kupungua kwa rutuba ya ardhi, upepo, joto, ukame na ukosefu wa aina ya mbegu bora za nyanya zenye mavuno mengi amabazo zinahimili mazingira ya kwetu, wadudu, magonjwa na magugu.


Ustawi:
Nyanya hustawi vizuri zaidi kwenye mazingira ya joto la wastani kuanzia nyuzi joto 18-27 sentigreti. Mvua nyingi husababisha mlipuko wa magonjwa ya ukungu kama vile Baka jani chelewa n.k.)

Rutuba ya udongo:

Nyanya hustawi kwenye aina zote za udongo kuanzia udongo wa kichanga, mweupe wa tifutifu hadi udongo wa mfinyanzi, ili mradi uwe na mboji ya kutosha na usiosimamisha/tuamisha maji. Pia uwe na uchachu wa wastani yaani pH 6.0 - 7.0.

Aina ya nyanya:
Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, nyanya hugawanywa katika makundi mawili stahimilifu.

Makundi ya nyanya:

Nyanya ipo katika makundi mawili kutokana na uchavushaji:
Mambo ya kuzingatia katika kilimo bora cha nyanya:

Kitalu:

Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya


Aina ya matuta:

– matuta ya makingo (sunken seed bed)
– matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed)
– matuta ya kawaida (flat seed bed)

Mambo ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta:


Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu:


1. Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed);


Faida:



Hasara:



2. Matuta ya makingo (sunken seed beds):


Faida:



Hasara:



3. Matuta ya kawaida (flat seed beds):


Faida:



Hasara:




Kusia Mbegu


  • Hakikisha ubora na uotaji wa mbegu kabla ya kuzipanda kitaluni (germination test)
  • Weka mistari kwenye tuta kulingana na ukubwa wa tuta, lakini mistari isiwe chini au zaidi ya sentimita 15-20 toka mstari hadi mstari
  • Kina cha mistari kisiwe cha kutisha bali kiwe kati ya sentimita 1-2
  • Matuta yapate maji ya kutosha siku moja kabla ya kusia mbegu. Ni vizuri kutumia chombo cha kumwagilia (watering can).
  • Mbegu ziatikwe kwenye mistari na zisambazwe vizuri ili kufanikisha usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta. Changanya mchanga laini na mbegu kisha sambaza kwenye mistari iliyoandaliwa kwenye tuta.
Mbegu zinaweza pia kuatikwa kwenye tuta bila mistari, lakini zisambazwe kwa uwiano mzuri kwenye tuta ili kupunguza msongamano. Msongamano husabisha magonjwa ya fangasi kama vile kinyausi (damping off) au ukungu (blight).

  • Weka matandazo kiasi cha kutosha ambacho hakitazuia kuota kwa mbegu.
  • Mara baada ya kuatika mbegu, mwagilia maji kiasi cha kutosha kulingana na unyevu nyevu ulioko ardhini
Mambo ya Kuzingatia baada ya kusia mbegu pamoja na Matunzo Kitaluni

  • Mwagilia maji kwenye kitalu baada ya kuotesha kulingana na unyevu nyevu uliopo kwenye udongo.
  • Miche yote ikisha ota, ondoa matandazo, kisha weka chanja ili kupunguza mionzi ya jua ambayo inaweza kuunguza miche michanga. (kipindi cha baridi si muhimu sana)
  • Punguzia miche (thinning) ili ibakie kwenye nafasi ya kutosha. Hivyo miche ibakie kwenye umbali wa sentimita 2.5 - 4. Hii itapunguza magonjwa ya ulemavu na mnyauko, pia itasaidia kupata miche bora na yenye nguvu.
  • Endelea kumwagilia hadi miche ifikie kimo kinachofaa kuhamishia shambani.
  • Punguza kiwango cha umwagiliaji maji, siku chache kabla ya kuhamishia miche shambani, yaani siku 7-10.

Kanuni na Mbinu za kuhamisha miche toka Kitaluni kwenda shambani (Transplanting
Rules)


  • Mwagilia miche masaa machache kabla ya kuhamishia miche shambani ili wakati wa kung’oa miche mizizi ishikamane vizuri na udongo.
  • Kabla ya kuhamisha miche, mashimo yawe yamekwisha andaliwa katika nafasi zinazo stahili huko shambani.
  • Miche ihamishwe wakati wa jioni ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na jua.
  • Kwa ujumla karibu mazao yote ya mboga mboga huwa tayari kuhamishiwa shambani yakiwa na majani kamili kati ya 2-6 pamoja na mizizi mingi iliyostawi vizuri.
  • Mche lazima uwe na afya nzuri, uwe umenyooka vizuri, hivyo miche yote iliyonyongea au myembamba kupita kiasi isichukuliwe wakati wa kupeleka shambani.
  • Ng’oa miche kwa uangalifu hasa pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
  • Miche ihamishiwe shambani mapema mara baada ya kung’olewa toka kitaluni.
  • Wakati wa kuhamisha miche, uangalifu mkubwa utumike ili kutoharibu miche/mizizi.


Maandalizi ya Shamba la Nyanya



  • Shamba la nyanya liandaliwe mwezi 1-2 kabla ya kupanda miche.
  • Mara baada ya kulima choma nyasi juu ya udongo au ondoa magugu yote yanayoweza kuhifadhi wadudu na magonjwa ya nyanya.
  • Siku moja au mbili kabla ya kuhamishia nyanya shambani, mwagilia sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuhamishia nyanya.
  • Nafasi kati ya mche hadi mche ni wastani wa sentimita (50-60) x (50-75) kutegemeana na aina au hali ya hewa. Kama ni kipindi cha baridi ni vyema nyanya zikapandwa mbalimbali ili kuruhusu mzungungo wa hewa na kuzuia magonjwa ya fangasi.

Jinsi ya kupanda miche:


  • Hamisha miche toka kitaluni pamoja na udongo wake
  • Sambaza mizizi vizuri kwenye shimo bila kukunja.
  • Fukia miche kina kile kile ambacho shina lilikuwa limefukiwa bustanini.
  • Mwagilia maji ya kutosha kulingana na unyevunyevu uliopo kwenye udongo kasha weka matandazo na kivuli ili kupunguza uharibifu unaosababishwa na mionzi ya jua.

Mambo muhimu ya kuzingatia baada ya kuhamishia Miche Shambani



  • Kagua shamba mara kwa mara ili kujua maendeleo au matatizo yaliyoko shambani mapema
  • Hakikisha shamba ni safi wakati wote, palilia shamba na hakikisha magugu yote hasa yale ya jamii ya nyanya yamelimiwa chini.
  • Ondoa mimea iliyoshambuliwa na magonjwa au ondoa sehemu zilizoshambuliwa, kisha zifukiwe chini au kuunguza moto.
  • Punguza matawi na vikonyo ili kuongeza mwanga wa kutosha kwenye nyanya pamoja na kuruhusu mzunguko wa kutosha wa upepo na kusababisha mazingira magumu ya wadudu maadui kwenye nyanya, hasa wale wanaopenda kiza na magonjwa yanayopendelea unyevunyevu.


Friday 15 August 2014

MKUU WA MKOA WA NJOMBE ATAKA TRA NA TFDA WASHIRIKIANE‏ AKIWA KATIKA ZIARA YA KUTEMBELEA MABANDA YA NANE NANE MBEYA.


  Banda la Tanseed katika maonesho ya nanenane.


 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kepten Mstaafu Aseri Msangi akipata maelezo mbali mbali katika Banda la Tanseed.
 Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Nyanda za juu kusini Rodney Alananga akimuonesha Mkuu wa Mkoa baadhi ya bidhaa feki ambazo hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Mkuu wa Mkoa akiangalia kiroba cha Konyagi kilichobandikwa nembo feki ya TRA.
 Afisa elimu kwa Mlipa kodi (TRA)wa Mkoa wa Iringa, Masunga Faustine  akikichunguza kwa makini kiroba cha Konyagi ili kuangalia namna ilivyochakachuliwa.
Maafisa wa TRA wakifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

***************
MKUU wa Mkoa wa Njombe, Kepteni Mstaafu Aseri Msangi, ameziagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya udhibiti wa chakula na dawa(TFDA) kuwa na mahusiano ya karibu.
 
Agizo hilo alilitoa jana katika ziara ya kutembelea mabanda ya maonesho ya wakulima nanenane yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
 
Msangi alisema kukiwa na mahusiano mazuri baina ya mamlaka hizo mbili kutachangia kudhibiti uingiaji na matumizi ya bidhaa feki hapa nchini.
 
Aidha alilazimika kutoa agizo hilo baada ya Tfda kubaini matumizi ya nembo ya TRA katika vinywaji vikali vinavyozalishwa na Konyagi kutumika katika pombe feki.
 
Katika ziara hiyo ambayo Mkuu wa Mkoa huyo alipitia mabanda ya Tra na Tfda alibaini kutokuwa na mahusiano na ushirikiano kutokana na Afisa wa Tra kushindwa kuigundua nembo yao kama ni Feki.
 
Akifafanua mbele ya Mkuu wa Mkoa kuhusu pombe feki, Kaimu Meneja wa TFDA kanda ya Nyanda za juu kusini, Rodney Alananga, alisema mbali na Serikali kupiga marufuku uingizwaji na matumizi ya Pombe kali kutoka nje ya nchi lakini pia imegundulika kuchakachuliwa kwa pombe za ndani.
 
Alananga alitolea mfano ni pombe aina ya Konyagi inayozalishwa na kampuni ya Tanzania Distillers Limited(TDL)kuwa wafanyabiashara wanafoji nembo ya TRA inayopaswa kubandikwa kwenye chupa na karatasi la kinywaji hicho.
 
Alizitaja baadhi ya sifa zilizokutwa katika pombe iliyochakachuliwa kuwa ni pamoja na utoafuti wa ujazo ulioandikwa kwenye nembo ya TRA na Nembo ya Kiwanda ambapo Kiwanda kimeandika ujazo wa ml 100 na kwenye nembo ikisomeka Ml 10.
 
Tofauti zingine ni pamoja na kutofautiana kwa jina la kiwanda, jina la bidhaa na biashara kukosekana kwa tarehe ya kuanza kutumika na mwisho wake pamoja na nembo hiyo feki kufutika kirahisi kuliko nembo halisi.
 
Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipa Kodi Mkoa wa Iringa, Faustin Masunga, alikiri kutojua tofauti hizo na kuahidi kuzidi kutoa elimu kwa wananchi ili kuepuka kuhatarisha afya za watu.
 
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kapt Mstaafu Aseri Msangi aliiagiza Mamlaka ya mapato (TRA) kujikita katika uoaji wa elimu kwa wanunuzi na walaji ili kuongeza ukusanyaji wa mapato.
 
Alisema endapo mnunuzi ataelimishwa juu ya sheria ya kodi(EFD Regulation ya Mwaka 2010) ya kumtaka anaponunua kitu adai risiti itasaidia kuongeza kwa ukusanyaji wa mapato nchini.
 
Alisema katika utoaji wa elimu wanapaswa kufuata mfumo wa Serikali ambao hutaka kumshirikisha kuanzia ngazi ya kijiji hadi ngazi za juu ambao ndiyo wenye watu na wanaopaswa kukusanya watu endapo watataka kutoa elimu.
 
Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Mkoa pia alitembelea mabanda ya kuzalisha mbegu ya Tanseed, Bodi ya Pareto,Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe, Mamlaka ya hali ya hewa na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.

by; kilimo tija

Tuesday 17 December 2013

ALUMINIUM AFRICA ( ALAF ) YATAMBULISHA BIDHAA MPYA KWA WAKANDARASI JIJINI MBEYA


Wadau wa sekta ya ujenzi hususani Makandarasi na mawakala wa vifaa vya ujenzi wakiwa makini kusikiliza utambuzi wa bidhaa za ALAF. mbele katikati (2) ni wanahabari wa Mbeya highlands fm wakiwa ni moja kati ya wanaofanya wasikilizaji kutambua ubra wa bidhaa hizo za ALAF


Meneja wa tawi la ALAF Mkoani Mbeya, Grayson Mwakasege, alisema lengo la mkutano huo ni kushirikisha wadau kuhusu bidhaa zao mpya ili wajue namna ya kuzitumia na siyo kukutana nazo sokoni bila taarifa yoyote.

Shailesh Tripathi
Manager pre Engineering Struchures



Picha ya pamoja baada ya hafla.



KAMPUNI ya ALAF LIMITED inayozalisha bidhaa mbali mbali za ujenzi kwa kutumia Vyuma, imekutana na wanahabari na wadau wa sekta ya ujenzi hususani Makandarasi na mawakala wa vifaa vya ujenzi ili kutambulisha bidhaa mpya pamoja na kupokea maoni juu ya uboreshaji wa bidhaa hizo.

Mkutano huo ulifanyika ijumaa 13.12.2013 katika ukumbi wa Hoteli ya GR City iliyopo Soweto Jijini Mbeya, ambapo uongozi wa Kampuni ya ALAF uliwaambia wadau bidhaa wanazozalisha kuwa ni Mabati maarufu kwa simba dumu ambayo wadau hao walielezwa namna ya kutofautisha na mabati feki yanayotolewa na watu wengine.

Meneja wa tawi la ALAF Mkoani Mbeya, Grayson Mwakasege, alisema lengo la mkutano huo ni kushirikisha wadau kuhusu bidhaa zao mpya ili wajue namna ya kuzitumia na siyo kukutana nazo sokoni bila taarifa yoyote.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na Scafolding, Ultra-span (vyuma vya makenchi) na bati za rangi mbali mbali kutoka Afrika Kusini ambapo washiriki wa Mkutano huo waliweza kutoa changamoto wanazokutana nazo wakati wa matumizi ya bidhaa hizo.

Wadau hao walisema changamoto kubwa ni bei ya bidhaa tofauti na vifaa vingine jambo ambalo lilibainika kuwa ni kutokana na malighafi wanazotengenezea yaani Chuma kutolewa nchini Japan na kusafirishwa hadi Dar Es Salaam ambako kipo kiwanda.

Kutokana na changamoto hiyo wadau hao waliishauri kampuni ya Alaf kuchangamkia madini yaliyogunduliwa Mchuchuma ili kupunguza gharama kwa wananchi kwa kuwa malighafi ya chuma itakuwa ikichimbwa hapa hapa nchini.

Mwakasege aliwashauri wananchi na watumiaji wa bidhaa zao kununua kutoka kwa mawakala waliowateua ili kuepuka kununua bidhaa feki.
Mawakala hao ni  Suju Hardware, TAFISA, Machemba na Ballus.

Aliongeza kuwa pia kampuni yao imeanza kuzalisha Ultra- Span ( vyuma vya kuezekea) badala ya matumizi ya mbao kwa madai kuwa itasaidia utunzaji wa mazingira kwa kutokata miti ovyo na kuimarisha nyumba zao kutokana na majanga ya moto na kuezuliwa na upepo.

Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ni Bati, Tiles, Pipes, Contena(moveble house) na mirunda ya Chuma badala ya kutumia miti.

92.7 Mbeya highlands fm radio

Tuesday 30 July 2013

KILIMO BORA CHA MIHOGO

Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  1. Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
    • Naliendele
                 Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.



    • Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9toka ipandwe.

  1. Mbinu bora za kilimo cha muhogo
    • Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
- Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta
·         Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
·         Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
-          Kulaza ardhini (Horizontal)
-          Kusimamisha wima (Vertcal)
-          Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
 Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.


·         Palizi:
-          Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
-          Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
-          Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
-          Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

·         Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

·         Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
-          Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
-          Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
-          Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
-          Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
-          Kwa kutumia mashine aina ya chipper
-          Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

Matumizi ya Muhogo
-          Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
-          Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
-          Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  
iii         MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
·         Magonjwa
Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia
      katika    muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu  chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

            Visababishi:
            Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

Dalili za Ugonjwa
Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

-          Kwenye majani
Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

-          Kwenye shina
Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.

-          Kwenye mizizi
Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.

Uambukizaji na ueneaji

Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika  katika hatua za mwanzo.
Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

Udhibiti/Kuzuia
ü  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.
ü  Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.
ü  Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.
ü  Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.
ü  Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
ü  Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.
ü  Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD
      


b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
      Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula  duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

Visababishi
Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa  kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).
Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
·         Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus
·        Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)
·         Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)


                  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
                  
                  Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri         
                   Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za    
                  Awali za ukuaji wa jani.
                  Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
                  tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
                
                  Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
                  Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
                  Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
                  Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
                  yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

                 Uambukizaji na uenezaji
                  Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida
                  hutumika kuzalishia mmea.
                  Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au
                  Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo
                  katika nchi za Afrika na India
                  Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika
                  Maeneo mapya.



                
 UHIBITI NA KUZUIA
                  -Hatua ya msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa
                   Mmea ambao hauna uambukizo wowote.
                  -Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile
                   Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
                  -Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD
                   inaangamizwa kwa kuchomwa moto.
                  -Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu waenezao CMD.
                  -Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

·         WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU
-          Cassava Mealy Bug (CMB)

Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.

-          Cassava Green Mites (CGM)

Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.

-          White Scales


Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

-          Mchwa
Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
-          Wanyama waharibifu
Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

Udhibiti/Kuzuia
Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
ü  Kutumia dawa za kuulia wadudu
ü  Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
      Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.