Tuesday, 30 July 2013

KILIMO BORA CHA MIHOGO

Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na mazao mengine kama vile kunde, mbaazi, njugumawe, n.k. Umuhimu wa zao hili ni kutupatia cahakula na wakati mwingine kwa biashara. Kwa kanda ya kusini muhogo ni chakula kikuu ambacho kinachukua asilimia 75 ya chakula kwa maeneo yote ya mikoa ya pwani

Muhogo hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye maeneo ya mita 0 – 1500 kutoka usawa wa bahari. Vile vile muhogo hustawi vizuri kwenye maeneo yanayopata mvua ya wastani wa mm 750  - mm1200 kwa mwaka. Muhogo hustawi vizuri kwenye ardhi ya kichanga. Vili vile zao la muhogo ni maarufu sana kwa uvumilivu wa hali ya ukame.

TEKNOLOJIA ZILIZOPO
  1. Mbegu bora za muhogo
Mpaka sasa hivi kuna aina mbili za mbegu bora ambazo zimathibitishwa kwa wakulima. Mbegu hizi huvumilia magonjwa, (batobato na matekenya), pia huzaa sana ukilinganisha na mbegu za kienyeji.
    • Naliendele
                 Huzaa tani 19 kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.



    • Kiroba
Huzaa tani 25 – 30  kwa hekta moja, na inaweza kuvunwa kuanzia miezi 9toka ipandwe.

  1. Mbinu bora za kilimo cha muhogo
    • Uandaaji wa shamba
Shamba liandaliwe kabla ya msimu wa kuanza. Uandaaji wa shamba bora hufuata hatua zifuatazo:
- Kufyeka shamba
- Kung’a na kuchoma visiki
- Kulima na kutengeneza matuta
·         Uchaguzi wa mbegu bora za kupanda
Mbegu zinatakiwa zisiwe na magojwa yeyote, pia chagua mashina ambayo yamelomaa vizuri.
·         Upanadaji
Kuna njia tatu za upandaji wa muhogo:
-          Kulaza ardhini (Horizontal)
-          Kusimamisha wima (Vertcal)
-          Kuinamisha ( Inclined/Slunted)

Urefu wa kipande cha shina cha kupanda:
 Inashauriwa urefu uwe sm 30; lakini urefu wa kipande cha kupanda unategemea sana idadi ya macho yaliyopo kwenye hicho kipande, inashauriwa kipande kiwe na macho (4 – 6).

Nafasi ya kupanda:
Kwa upandaji wa shamba muhogo tupu, shina hadi shina ni mita 1 na mstari hadi mstari ni mita 1.Kwa shamba la mchanganyiko na mazao mengine, inategemeana na zao linalochanganywa; mstari hadi mstari ni mita 2 – mita 4 na shina hadi shina ni mita 1.


·         Palizi:
-          Palizi ya kwanza ifanyike mapema (mwezi 1) baada ya kupanda ili kuepukana na magugu yanayochipua haraka baada ya mvua kunyesha. Ndani ya miezi mine ya mwanzo mihogo haitakiwi kuwa na magugu ili kuepuka ushindni wa mahitaji muhimu (mwanga, mbolea, maji, n.k) kati ya muhugo na magugu.
-          Palizi hufanyika kwa kutumi jebe la mkono au dawa ya kuuwa magugu.
-          Wakati mwingine udhibiti wa magugu kufanyika kwa kutumia majani kwa kutandazwa juu ya udongo.
-          Plaizi hufanyika mara 2 – 3 hadi muhugo kukomaa.

·         Uvunaji:
Mihogo inaweza kuanza kuvunwa baada ya miezi 9 – 12 tangu kupandwa. Inashauriwa kuvuna katika katika kipindi cha jua; kwani wakati wa mvua kiwango cha wanga kwenye muhogo hupungua.

·         Usindikaji bora
Usindikaji bora wa muhogo unafanyika kwa sababu kuu mbili:
-          Kurahisisha/kuharakisha ukaushaji
-          Kuondoa sumu (cyanide) ilyoko kwenye baadhi ya aina za mihogo
-          Kuongeza ubora wa unga utokanao muhogo wenyewe.

Njia bora za usindikaji
-          Kwa kutumia mashine aina ya Grater
Hii hutoa chembechembe laini za muhogo, ambazo baadae hukamuliwa kwa kutumia kifaa kingine kiitwacho “presser” ili kuondo sumu iliyoko kwenye muhogo. Mashine hii hutumika hususani kwa muhogo mchungu.
-          Kwa kutumia mashine aina ya chipper
-          Mashine hii hutoa vipande vidogo vidogo (chips). Mashine hii hutumika hasa hasa kwa ajili ya mihogo mitamu/baridi.

Matumizi ya Muhogo
-          Muhogo unaweza kupikwa wenyewe kama chakula au kutengeneza unga
-          Unga wa muhogo unaweza kutengeneza vitu vyotekama vinavyotengenezwa na unga wa ngano kama vile biskuti, chapatti, maandazi, chichili, keki n.k.
-          Pia muhogo huweza kutumika viwandani kutengeneza bidhaa nyingine kama vile wanga.

  
iii         MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU
·         Magonjwa
Kuna magonjwa mawili ambayo ni muhimu sana na yanapunguza uzalishaji wa zao la muhogo.
a) Ugonjwa wa Matekenya au Ugonjwa wa michirizi ya kahawia
      katika    muhogo
  Ugonjwa huu ni maarufu kwenye sehemu zenye miinuko iliyo na urefu  chini ya mita 300 na unapatikana kidogo sana kwenye miinuko ya mita 500 na kuendelea ambako uenezaji wake wa kawaida hautokei kabisa.

            Visababishi:
            Matokeo ya uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba ugonjwa huu ulienezwa na mdudu mweuupe au inzi mweupe (whitefly) mwenye mabawa madogo.

Dalili za Ugonjwa
Sehemui zote za muhogo zinaweza kuonyesha dalili za uambukizo wa ugonjwa huu lakini ni vipengele gani vya ugonjwa na ni kwa kiwango gani hutegemea hali ya mzingira, hatua ya kukua kwa mmea kwa kulinganisha.

-          Kwenye majani
Dalili ya kwanza: Chlorosis rangi ya njani hutokea kwanza pembezoni mwa vena ndogo baadae huathtiri vena ndogo zaidi na inaweza kuwa doa (chlorosis) la rangi ya njano.
Dalili ya pili: Rangi ya njano ambayo haihusishwi vizuri na vena isipokuwa katika mbaka ya mviringo kati ya vena kuu kwenye hatua za mwisho za ugonjwa sehemu kubwa ya lamin inaweza isiathirike, majni yenye ugonjwa hubaki yameshikilia kwenye mmea kwa muda wa wiki kadhaa.

-          Kwenye shina
Huonekana kwenye tisu ya shina changa la kijani, jeraha la zambarau au kahawia linweza kuoneakan nje na kuingia ndani hadi kwenye gamba baaada ya kubandua gome la nje. Pia jeraha la nekrotiki kwenye kovu la shina hutokea baada ya majni kudondoka kutokana na umri wa mmea. Tawi/shina hufa kuanzia kwenye nch kuelekea chini na kusababisha kufa kwa mmea wote.

-          Kwenye mizizi
Kwa kawaida hutokea baada ya dalili za majani na wakati wa kipindi kati ya uambukizo na kufa, amabpo kifo cha mizizi hutokea kuanzia miezi 5 toka kupandwa. Dalili za mizizi zinabadilika nje ya mizizi na zinaweza kuwa kamakizuizimwanga au shimo au kufa kwenye gome.

Tishu inayo zunguka mshins ina doa la rangi ya kahawia au nyeusi. Wakati mwingine mizizi huonekana kuwa yenye afya kwa nje bila kuwa na matatizo yaliyowazi au bila kupungua ukubwa, lakini ikikatwa huonekana kufainakufa au rangi ya njano.

Uambukizaji na ueneaji

Ugonjwa wa CBSD unaambukizwa kwa njia ya vipandikizi vinavyotokea kwenye mimea iliyoathiriwa vinavyosababisha mmea kuonesha kwenye majani dalili za ugonjwa.
Kwa kuwa muhogo kwa kawaida huzalishwa kwa njia ya vipandikizi ugonjwa huu huingizwa kwenye sehemu mpya zilizopandwa kwa kutumia vipandikizi vilivyoambukizwa.
Kwa aina zinazovumilia sana kwenye hali za mabondeni, dalili mbaya sanahutokea wakati ugonjwa ukigundulika  katika hatua za mwanzo.
Uchunguzi umeonesha kwamba Bemisia afer ni mdudu/kisababishi ambacho ndicho kinachohusiana na maendeleo ya hivi karibuni kuhusu uhamishaji wa visababishi kama “ipomovirus”. Mara nyingine inaonesha nzi weupe (White flies) na kutokana na hali hiyo bado uchunguzi unaendelea zaidi.

Udhibiti/Kuzuia
ü  Njia ya msingi ya kuzuia/kudhibiti ugonjwa wa CBSD ni kuchagua mbegu kutoka kwenye mimea isiyo na dalili ya ugonjwa.
ü  Ubora wa mashina unahitaji kutunzwa kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza ile iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua.
ü  Hakikisha kuwa unapanda mbegu bora za mhogo ambazo zinastahimili uambukizo wa magonjwa.
ü  Hakikisha kuwa wakati wa uvunaji uonapo hali ya kuoza kwa mizizi ya mhogo ichome moto ili kutokomeza ugonjwa huo.
ü  Kuelewa dalili za ugonjwa wa CBSD kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya kutokomeza ugonjwa huu.
ü  Hakikisha kuwa unaendelea kutunza mbegu bora zinazoonekana kuvumilia magonjwa sana.
ü  Hakikisha kuwa shamba la mhogo linakuwa safi kwa ajili ya kupunguza visababishi vya ugonjwa wa CBSD
      


b) Ugonjwa wa batobato au ukoma wa majani
      Ni ugonjwa ambao ulienezwa kwamara ya kwanza hapa Tanzani mwaka 1894, na baadae uliripotiwa katika nchi nyingine nyingi za Afrika Mashriki, Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na sasa unafahamika kuwa upo maeneo yote yanayolimwa muhogo Afrika.

Katika viwango vya kuwepo kwa ugonjwa wa CMD na katika uwingi wa hasara zinazopatikana kutokana na CMD ni kati ya 15% – 20%. Hii ni sawa na tani milioni 15 – 18 zikilinganishwa na makadirio ya shirika la kilimo na chakula  duniani ya tani milioni 85 ya mwaka 1997.

Visababishi
Tangu ugonjwa wa CMD ulipoenezwa kwa mara ya kwanza, visababishi vilichukuliwa  kuwa ni virusi kwa sababu ya kukosekana kisababishi kingine. Kwa hiyo kutokana na kuwa mtazamo huu unalingana na matokeo ya uchunguzi wa awali inaonesha kwamba ugonjwa huu huenezwa na nzi mweupe (white fly).
Pia uchunguzi wa mara kwa mara umesababisha utambuzi wa virusi vya aina mbalimbali na tofauti kama ifuatavyo:
·         Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Africa cassava mosaic virus
·        Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya Afrika mashariki (East Africa cassava mosaic virus)
·         Ugonjwa wa batobato unaosababishwa na virusi vya India (Indian cassava mosaic virus)


                  Dalili za ugonjwa wa batobato (Cassava Mosaic Disease-CMD)
                  
                  Dalili hutokea kwenye jani lenye uwaraza wa michirizi ambazo huathiri         
                   Sehemu zisizokunjamana za kutolea hewa na hufahamika katika hatua za    
                  Awali za ukuaji wa jani.
                  Sehemu za kloritiki hushindwa kutanuka hadi mwisho, hivyo mvutano unaji-
                  tokeza kutokana na ukuaji usiolingana na jani au majani madogo yaliyoharibika.
                
                  Majani yaliyoathirika sana hupungua ukubwa wa umbo, na hujikunja na kujitenga kwa
                  Sehemu zenye rangi ya njano na zenye rangi ya kawaida ya kijani.
                  Mmea hudumaa na majani machanga hupatwa na uvimbe.
                  Kloritiki ya jani inaweza kuwa ya rangi ya manjano nyepesi au rangi inayokaribia nyeupe
                  yenye kijani kidogo au kupauka kuliko ilivyo kawaida.

                 Uambukizaji na uenezaji
                  Ukoma wa mhogo huambukizwa kwenye vipandikizi vya shina ambavyo kwa kawaida
                  hutumika kuzalishia mmea.
                  Pia huenezwa na inzi mweupe (white fly) aitwae Bemisia tabaci G. Aina mbili za inzi au
                  Mbu hao Bemisia (Preisner Hhosny na Aleorodius disperses R) pia huambukiza mihogo
                  katika nchi za Afrika na India
                  Usambazaji wa vipandikizi unaweza kusababisha kuenea kwa ugonjwa wa CMD katika
                  Maeneo mapya.



                
 UHIBITI NA KUZUIA
                  -Hatua ya msingi ya kuzuia ugonjwa wa CMD ni kwa kuchagua vipandikizi kutoka kwa
                   Mmea ambao hauna uambukizo wowote.
                  -Ubora wa mashina unahitajika kwa kuendelea kuchagua na kuangamiza kwa kung’oa ile
                   Mihogo iliyoambukizwa ambayo inaonekana wakati wa kuchipua
                  -Hakikisha kuwa wakati wa kuvuna mihogo kwa ile iliyoathirika na ugonjwa wa CMD
                   inaangamizwa kwa kuchomwa moto.
                  -Hakikisha kuwa unatunza shamba na kuwa safi ili kupunguza wadudu waenezao CMD.
                  -Hakikisha una elimu ya kutosha juu ya dalili za ugonjwa wa CMD>

·         WADUDU NA WANYAMA WAHARIBIFU
-          Cassava Mealy Bug (CMB)

Wadudu hawa hushambulia kwenye ncha za mashina/matawi kwenye majani machanga. Athari zake ni kwamba majani ynadumaa na kujikusanya pamoja, hivyo basi kupunguza ukuaji wa mmea kwa ujumla. Vile vile urefu kati ya pingili na pingili huwa fupi sana.

-          Cassava Green Mites (CGM)

Wadudu hawa hushambulia majani mapya sehemu za chini. Madhara yake sio makubwa.

-          White Scales


Hawa ni weupe na hujishika kwenye shina na kufyonza maji kutoka kwenye mti wa muhogo. Vili vile wadudu hawa madhara yake sio muhimu.

-          Mchwa
Hawa hutafuna/hula mashina ya muhogo hasa wakati wa jua kali/kiangazi.
-          Wanyama waharibifu
Hawa hushambulia muhogo ukiwa shambani kwa kuula, kama vile nguruwe, panya, wezi, n.k

Udhibiti/Kuzuia
Kwa upande wa wadudu wanweza kudhibitiwa kwa njia zifuatazo:
ü  Kutumia dawa za kuulia wadudu
ü  Kutumia wadudu marafiki wa wakulima
      Kwa upande wa wanyama ni kuweka walinzi.


Monday, 13 May 2013

FANYA MAHARAGE IWE MKOMBOZI


MBEGU BORA ZA MAHARAGE

Aina mbili ya mbegu bora za maharage zimeendelezwa/zimezalishwa katika kituo cha utafiti wa kilimo kilichopo Uyole mkoani mbeya. Mbegu hizo ni BILFA 16 na UYOLE 04. Kuzalishwa kwa mbegu hizi bora ni juhudi za muda mrefu za mpango wa kuzalisha mbegu bora za maharage lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji na maharage yakiwa katika sifa na ubora unapendekezwa na wakulima pamoja na walaji, wakulima hupendelea mbegu zinazohimili magonjwa, zinazohimili ukame na zenye mazao mengi wakati walaji hupendelea maharage yenye ladha nzuri na yanayoiva kwa urahisi yakiwa katika bei yenye unafuu.

Mbegu ya UYOLE 04 hutambaa, huzaa maharage yenye ukubwa wa wastani mpaka kubwa kabisa zikiwa na rangi ya maziwa, zinahimili magonjwa sugu kama kutu ya maharage na anthracnose, huiva haraka yakipikwa na huwa na ladha nzuri sana

Wakati wa kupanda mbegu hii hutegemea msimu wa kuanza na kuisha kwa mvua, kwa mfano sehemu ambazo mvua huisha mwisho wa mwezi wa 4 au mwanzo wa mwezi wa 5 basi upandaji uanze mwezi wa 3 kwa sababu ukuaji wa mbegu hizi mpaka kukomaa huchukua wastani wa siku 105. Kiasi cha mbegu zinazohitajika kupanda ni kilo 70 – 80kwa hekta ambapo miche 200,000 huota na huweza kuzalisha kiasi cha tani 1.5 – 1.8kwa kila hecta, mbegu hii hufaa sana kupandwa nyanda za juu kaskazini (mikoa ya Mbeya, Iringa, Songea na Rukwa) ambako ardhi imeinuka wastani wa mita 800 – 2000kutoka usawa wa bahari na kuna baridi.


BILFA 16

Mbegu ya BILFA 16 huwa na rangi nyekundu mchanganyiko na maziwa kama nguo ya jeshi, mbegu ni za ukubwa wa wastani, huweza kuhimili sana magonjwa, mimea ni ya kijani kibichi yenye majani madogo madogo huwa na matawi 4 – 5 maua huwa na rangi ya pinki na vishubaka vya maharage huwa vyeupe na vikikomaa huwa rangi ya maziwa

. Kiasi cha mbegu zinazohitajika kupanda ni kilo 70 – 80 kwa hekta ambapo miche200,000 huota na huweza kuzalisha kiasi cha tani 1.2 – 1.5 kwa kila hecta, ambacho ni kidogo ukilinganisha na UYOLE 04, mbegu hii hufaa sana kupandwa nyanda za juu kaskazini (mikoa ya Mbeya, Iringa, Songea na Rukwa) ambako ardhi imeinuka wastani wa mita 800 – 2000 kutoka usawa wa bahari na kuna baridi. Na mbegu hii hukoma baada ya siku 80 – 84 tangu kupandwa kwa hiyo hufaa kwenye maeneo yenye mvua za muda mfupi

Friday, 10 May 2013

Utunzaji wa udongo kwa ajili ya kilimo hai



Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo.

Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo.

Utunzaji wa rutuba ya udongo unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo wenye rutuba utazalisha mimea yenye afya inayoweza kukabiliana na magonjwa. Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili uhakikisha kunakuwepo uzalishaji wa kutosha bila ya kutumia pembejeo za ziada isipokuwa matandazo, mboji na bila kutifua udongo mara kwa mara. Ongezeko la malighafi za asili husaidia kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa virutubisho vya kutosha.

Athari kwa afya ya mimea

Kwa bahati mbaya, aina ya kilimo cha kisasa na kinachotumia kemikali hufanywa tofauti na ilivyo kwa kilimo hai. Katika aina hii ya kilimo; udongo hulimwa mara kwa mara jambo linalosababisha uharibifu wa muundo wa udongo, uwiano wa virutubisho, ambapo virutubisho huongezwa kwa kutumia mbolea za viwandani na matandazo hayazingatiwi. Muundo wa udongo unapobadilika, rutuba nayo hupungua, uwezo wa udongo kwenye udongo pia hupungua.

Kiwango cha udongo mzuri pia hupungua kwa kuwa hakuna tena viumbe hai wanaotengeneza udongo ila unapungua kila msimu wa mavuno. Kwa asili mzunguko huu huwa na matokeo yanayoishia kwenye afya ya mimea, na hapa wadudu huchukua nafasi inayowawezesha kufikia malengo yao.

Ziba pengo

Wakulima wanatakiwa kuhakikisha kuwa kuna virutubisho vya kutosha shambani mwao kila wakati. Ikiwa kuna mwanya pale ambapo baadhi ya pembejeo zinakosekana, kununua virutubisho kwa ajili ya udongo vilivyomo kwenye mfumo wa mbolea za asili inaruhusiwa. Hata hivyo, weka utaratibu wa kuwa na virutubisho kutoka shambani mwako muda wote.

Endapo tukitegemea kulisha udongo kutokana na mbolea za viwandani na kutumia virutubisho vya asili, bado tutakuwa tunafanya sawa na yanayofanyika katika kilimo cha kisasa. Tutakuwa hatujauongezea udongo uwezo wa kujitengeneza na kuongezeka, jambo ambalo ndio msingi muhimu wa kilimo hai.

Vyanzo vya virutubisho

Mimea inayofunika udongo – Mimea inayotambaa huongeza na kushika virutubisho kwenye udongo, kuongeza malighafi zinazooza kwenye udongo, kuzuia madini ya naitraiti kuzama kwenye udongo, virutubisho kutiririshwa, na mmomonyoko wa udongo. Jambo la muhimu hapa ni kuwa udongo umefunikwa ili kuzuia uharibifu. Mimea jamii ya mikunde inapendekezwa zaidi kwa kuwa
husaidia kuongeza nitrojeni kwenye udongo inayopatikana hewani.

Inashauriwa pia kuchanganya mimea jamii ya mikunde na nyasi kwa kuwa nyasi hutumia nitrojeni nyingi sana kutoka kwenye udongo, hivyo itasaidia kutokuharibika kwa mtiririko mzima wa uwekaji wa nitrojeni kwenye udongo.

Mboji - Mboji hasa inayotengenezwa kwa kutumia kinyesi cha wanyama, inaweza kuwa chanzo kizuri cha viumbe wadogo kwenye udongo na virutubisho vyenye gharama ndogo. Unapotumia mboji, changamoto kubwa ni kuhakikisha kuwa imeoza vizuri na namna ya kuitumia kwa usahihi. Endapo mchanganyiko uliotumika kutengeneza mboji hiyo yalikuwa na ubora wa chini, basi mboji hiyo nayo itakuwa na ubora mdogo sana. Itakuwa vizuri kama wakulima hawataacha mboji ikapigwa na jua au mvua, kwa kuwa hali hii inaweza kusababisha kupotea kwa virutubisho kwenye mboji. Kinyesi cha mifugo huboresha mboji zaidi.

Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa kiasi cha 15% ya virutubisho vinavyopatikana kwenye mboji hutumika shambani kwa mwaka wa kwanza. Hivyo, matumizi ya mara kwa mara ya mboji yanapendekezwa ili kuweza kuongeza nitrojeni na malighafi zinazo oza kwenye udongo.

Samadi - Samadi inayotokana na wanyama waliokomaa inaweza kuwa na uwiano mzuri wa virutubisho vya nitrojeni na aina nyingine kwa kiasi kidogo. Tatizo moja la samadi ni upatikanaji pamoja na kutokuwa na ubora unaofanana wakati wote. Kiasi kikubwa cha samadi inayotumika kwenye shamba la mboga, huozeshwa kabla ya kutumika, jambo linalosaidia kupunguza madhara kwenye vyakula.

Malengo kwa ajili ya udongo na mazao
•  Kuongeza malighafi zinazo oza kwenye udongo
• Kuboresha muundo wa udongo
• Kuwezesha upatikanaji wa nitrojeni
• Kuongeza uwezo wa uhifadhi wa rutuba
• Kujenga uwepo wa uhai wa viumbe hai kwenye udongo
• Kufifisha magonjwa ya mazao
• Kujenga mazingira ya udongo wenye uwiano