Picha ya pamoja baada ya hafla.
KAMPUNI ya ALAF LIMITED inayozalisha bidhaa mbali mbali za ujenzi kwa kutumia Vyuma, imekutana na wanahabari na wadau wa sekta ya ujenzi hususani Makandarasi na mawakala wa vifaa vya ujenzi ili kutambulisha bidhaa mpya pamoja na kupokea maoni juu ya uboreshaji wa bidhaa hizo.
Mkutano huo ulifanyika ijumaa 13.12.2013 katika ukumbi wa Hoteli ya GR City iliyopo Soweto Jijini Mbeya, ambapo uongozi wa Kampuni ya ALAF uliwaambia wadau bidhaa wanazozalisha kuwa ni Mabati maarufu kwa simba dumu ambayo wadau hao walielezwa namna ya kutofautisha na mabati feki yanayotolewa na watu wengine.
Meneja wa tawi la ALAF Mkoani Mbeya, Grayson Mwakasege, alisema lengo la mkutano huo ni kushirikisha wadau kuhusu bidhaa zao mpya ili wajue namna ya kuzitumia na siyo kukutana nazo sokoni bila taarifa yoyote.
Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni pamoja na Scafolding, Ultra-span (vyuma vya makenchi) na bati za rangi mbali mbali kutoka Afrika Kusini ambapo washiriki wa Mkutano huo waliweza kutoa changamoto wanazokutana nazo wakati wa matumizi ya bidhaa hizo.
Wadau hao walisema changamoto kubwa ni bei ya bidhaa tofauti na vifaa vingine jambo ambalo lilibainika kuwa ni kutokana na malighafi wanazotengenezea yaani Chuma kutolewa nchini Japan na kusafirishwa hadi Dar Es Salaam ambako kipo kiwanda.
Kutokana na changamoto hiyo wadau hao waliishauri kampuni ya Alaf kuchangamkia madini yaliyogunduliwa Mchuchuma ili kupunguza gharama kwa wananchi kwa kuwa malighafi ya chuma itakuwa ikichimbwa hapa hapa nchini.
Mwakasege aliwashauri wananchi na watumiaji wa bidhaa zao kununua kutoka kwa mawakala waliowateua ili kuepuka kununua bidhaa feki.
Mawakala hao ni Suju Hardware, TAFISA, Machemba na Ballus.
Aliongeza kuwa pia kampuni yao imeanza kuzalisha Ultra- Span ( vyuma vya kuezekea) badala ya matumizi ya mbao kwa madai kuwa itasaidia utunzaji wa mazingira kwa kutokata miti ovyo na kuimarisha nyumba zao kutokana na majanga ya moto na kuezuliwa na upepo.
Baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ni Bati, Tiles, Pipes, Contena(moveble house) na mirunda ya Chuma badala ya kutumia miti.
92.7 Mbeya highlands fm radio
|