Sunday 28 April 2013

Akisoma hotuba ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Msemaji Mkuu wa mambo yanayohusu wizara hiyo, Rose Kamili alisema wanahitaji maelezo kwa sababu ni miaka michache imebaki kukamilika kwa utekelezaji huo




Mtoto akipalilia shamba la mpunga wilayani bariadi mkoa wa Simiyu hivi karibuni, mvua zinazoendelea kunyesha zinaleta matumaini ya kupatikana kwa chakula nchini katika msimu huu. Picha na Mpoki Bukuku


Kambi ya Upinzani Bungeni,imeitaka Serikali kueleza kwa kina utekelezaji wa nguzo kumi za Kilimo Kwanza, kwa kuzingatia kuwa imebaki miaka miwili kukamilika utekelezaji wa dhana hiyo.
Akisoma hotuba ya kambi hiyo kuhusu makadirio ya bajeti ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Msemaji Mkuu wa mambo yanayohusu wizara hiyo, Rose Kamili alisema wanahitaji maelezo kwa sababu ni miaka michache imebaki kukamilika kwa utekelezaji huo.
Kamili alitaja nguzo hizo kuwa ni dira ya kilimo kwanza, kugharimia kilimo, muundo mpya wa taasisi ya usimamizi, mabadiliko ya mfumo wa mkakati na ardhi kwa ajili ya kilimo.
Nyingine ni sayansi, teknolojia na rasilimali watu, miundombinu kwa ajili ya kilimo kwanza na uhamasishaji wa Watanzania kuhusu kilimo. Kamili alisema kambi ya upinzani inataka majibu ya kina kama Sh60 bilioni zilizotolewa badala ya Sh750 bilioni zilizopangwa kwa ajili ya uanzishaji wa Benki ya Kilimo, zitatosha kulingana na mpango wa utekelezaji.
“Pia, tunataka kujua kama mtaji huu wa Sh60 bilioni ni sehemu ya marejesho ya fedha za EPA kama Bunge lilivyokuwa limeelezwa kuwa fedha za EPA zitaelekezwa kwenye kilimo,” alisema Kamili.
Mbunge huyo alisema mwenendo wa kilimo nchini tangu mwaka 1996 kwenye uchumi wa nchi, umekuwa ukikua kati ya asilimia 3.5 na 7.8 kwa mwaka na kwamba hiyo inaonyesha kuwa kasi ya ukuaji inapungua

No comments:

Post a Comment